Tanzania kupitia timu ya taifa ‘Taifa Stars’ imeendelea kupaa kimataifa chini ya utambuzi wa Shirikisho la Soka Duniani ‘FIFA’, baada ya kupanda kwa viwango vya ubora ambavyo hutolewa na shirikisho hilo kila mwezi.

Orodha ya viwango vya ubora wa soka duniani iliyotolewa na ‘FIFA’ kwa mwezi huu Oktoba, inaonesha Tanzania imeshika nafasi ya 130 ikitoka nafasi ya 132, ikipanda kwa nafasi mbili juu tofauti na mwezi Septemba.

Ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Benin katika mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2022 kwa upande wa Bara la Afrika, uliochezwa Oktoba 10 umechochea kupanda kwa viwango kwa Tanzania katika orodha hiyo ya ubora wa soka duniani.

Tanzania imefika nafasi ya 132, ikijikuzanyia alama 1123.84 kutoka zile 1115.37 ilizokuwa nazo mwezi Septemba.

Wakati Tanzania ikipanda, nchi ya Kenya imeporomoka kwa nafasi mbili kutoka ile ya 102 waliyokuwepo awali hadi nafasi ya 104.

Rwanda imeanguka kwa nafasi tano kutoka ile ya 128 hadi nafasi ya 133 wakati Burundi imebaki katika nafasi ya 141 iliyokuwepo hapo awali.

Uganda imeendelea kuwa kinara kwa upande wa ukanda wa Afrika Mashariki baada ya kupanda kwa nafasi nne kutoka ile ya 86 hadi nafasi ya 82.

Wivu wa Mapenzi wamponza mtoto wa Floyd Mayweather
Shoga yangu alivyonichukulia Mume wangu