Timu ya Taifa ya Tanzania ya Soka kwa wenye Ulemavu (Tembo Warriors), imeipa hadhi nchi kwa kuwa Taifa la kwanza Afrika, kufuzu kwenda Robo Fainali za Michuano hiyo ‘CANAF’ ambayo Tanzania ni mwenyeji.

Tanzania imepata nafasi hiyo baada ya kuifunga Timu ngumu ya Taifa ya Sierra Leone bao 1-0 kwenye mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam, leo Jumanne (Novemba 30).

Akizungumza baada ya mchezo huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Michezo Tanzania, Dkt. Hassan Abbasi alisema: “Sasa tuna mechi moja mbele kabla ya kupata tiketi mbili muhimu, moja ni kuingia nusu fainali lakini tukishinda mechi hiyo moja pia tutakuwa tumefuzu moja kwa moja kwenda Kombe la Dunia litakalofanyika mwakani mjini Instanbul, Uturuki.”

RC Makalla atoa maagizo TMDA
Matola: Tutafanya mabadiliko ya kikosi