Tanzania imesema haikubaliani na hatua ya Rais wa Marekani, Donald Trump ya kuutambua mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesema kuwa inaunga mkono makubaliano ya kimataifa ambayo yanatambua haki ya watu wa Palestina kumiliki Mashariki mwa Jerusalem kama ilivyokuwa kwenye mpaka wa kabla ya mwaka 1967.

“Tanzania inaunga mkono msimamo wa Umoja wa Mataifa wa suluhu ya mataifa mawili ambayo unatoa nafasi ya Israel na Palestina kuwepo kwa pamoja zikiwa na mipaka salama,” imesema taarifa hiyo iliyotiwa saini na Waziri Augustine Mahiga.

Aidha, tofauti na hilo la kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel, Trump alisema kuwa Marekani pia itahamisha ubalozi wake kutoka Tel Aviv na kuhamishia Jerusalem kitu ambacho kimengwa vikali

Hata hivyo, Msimamo wa Tanzania unaenda sambamba na msimamo wa mataifa mengi ya Afrika pamoja na Tume ya Umoja wa Afrika (AU).

Muuaji wa Kili Stars awekwa kwenye orodha Msimbazi
Azam U-11, U-13 kushiriki Chipkizi Cup