Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Mhandisi James Kilaba ametaja mikoa sita nchini kuanza utekelezaji wa zoezi la kusajili laini za simu kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kielektroniki inayohusisha uchukuaji wa alama za vidole.

Leo hii katika viawanja vya Mlimani City amefanya uzinduzi wa mfumo huo na kuitaja mikoa hiyo kuwa ni Dar es salaam, Pwani, Iringa, Tanga, Singida na Zanzibar.

Amesema huduma hiyo inatokana na changamoto wanazokutana nazo katika swala zima la usimamiaji wa huduma hiyo.

Pia ameeleza kuwa kutokana na tabia iliyozuka juu ya udanganyifu hasa katika kutoa taarifa za wanaosajili namba zao huku baadhi wakitumia simu kufanya uhalifu.

”Kutokana na changamoto hizo za kuongezeka kwa watumiaji wa huduma hii kuna umuhimu wa kuwa na takwimu sahihi za watumiaji kwa ajili ya matumizi ya usiamamizi, kiuchumi na kiusalama” amesema Kilaba.

Aidha ameongezea kuwa mfumo huo pia utawezesha kuhusu watumiaji wa simu za mkononi kwa ajili ya kuweka mipango ya kuendeleza sekta ya mawasiliano.

Nape akana kuhusika na kinachoendelea nchini
Tanzia: Kiungo mchezaji wa Simba afariki dunia