Mbunge wa Jimbo la Mtama kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amesema kuwa hahusiki na chochote kinachoendelea nchini.

Ameyasema hayo mara baada ya kutuhumiwa na mwananchi mmoja kuhusika na matukio mbalimbali yanayoendelea nchini.

“Naamini unaitwa Kusiluka, nimesoma lawama zako kwangu, una haki ya kulaumu ili upumue, lakini kuna kikao nimeshiriki kupanga hayo unayonituhumu?! Nadhani kuwa mkweli kwa nafsi yako tuhuma hizo ni nzito si sawa kuzisema bila kuwa na hakika, sihusiki na hayo usemayo na nayalaani pia,”amesema Nnauye

Hata hivyo Nape amewataka Watanzania kwa pamoja kuwasha mishumaa ya matumaini na kwamba amani ipo ya kutosha nchini.

Mwananchi amemtuhumu kiongozi huyo kuwa anaelewa kinachoendelea nchini baada ya muendelezo wa matukio mbalimbali yanayoendelea nchini.

'Kibamia' yamtia kitanzini Roma Mkatoliki
TCRA: Usajili wa laini za simu kwa alama za vidole kuanza rasmi