Siku chache baada ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kufungia video ya wimbo wa AY aliomshirikisha Diamond, Zigo Remix, imekiri kuwa wimbo huo umevunja rekodi ya malalamiko waliyowahi kuyapata.

AY

Akizungumza hivi karibuni katika mkutano maalum kati ya Mamlaka hiyo na AY ofisini kwao jijini Dar es Salaam, Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungi alisema kuwa walibaini wimbo huo ulikuwa unapendwa sana.

“Wimbo huu ulikuwa kwenye demand kubwa, ukimwambia mtu autoe huu wimbo ni issue na unaona reaction ya watu,” alisema Mungi.

Afisa Mwandamizi, masuala ya utangazaji na maudhui, Andrew Kisaka ambaye aliongoza mkutano huo, alimuelezea AY sababu za kuifungia video hiyo kutochezwa mchana huku akinukuu vifungu vya sheria vilivyozingatiwa.

Baada ya mkutano huo, AY alieleza kuwa amekubaliana na Mamlaka hiyo kufanyia marekebisho baadhi ya sehemu kwenye video hiyo ili ipate nafasi ya kuchezwa muda wowote, tofauti na hivi sasa ilivyoamriwa kutooneshwa mchana kupitia vituo vya runinga nchini.

TCRA iliifungia video ya wimbo huo kutochezwa mchana wakieleza kuwa inakiuka maadili.

Video ya wimbo huo iliwekwa YouTube Januari 22 mwaka huu kupitia channel ya AY, na hadi leo imefikisha zaidi ya Views milioni tatu na laki tano.

Magufuli amuondoa Balozi Ombeni Sefue, ateua Katibu Kiongozi Mpya
TFF yapinga michezo ya Bahati Nasibu 'Betting'