Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia, Selestin Kakele amesema maoni chanya yanatakiwa katika matumizi ya TEHAMA, ili kuboresha maisha ya Watanzania katika ulimwengu wa kidigitali.
Kakele ameyabainisha hayo jijini Dar es Salaam wakati akifungua kikao cha kutoa maoni kuhusu ya sera ya Taifa ya TEHAMA kwa ajili ya makundi anuai na kudai kuwa ipo haja ya kufanya marejeo ya sera ya TEHAMA kwa kuzingatia taratibu za uandaaju na sharti la msingi la ushirikwishaji wa jamii.
Amesema, “Sera ya TEHAMA ya mwaka 2016 ni ya mda mrefu, TEHAMA kama kiumbe ambacho kinazaliwa kinakua na kinabadilika kulingana na wakati pia mambo mbalimbali yanatokea duniani na yqnabadilika katika jamii hivyo upo umuhimu wa kufanya marekebisho.”
Aidha, Kakele ameongeza kuwa wakati wanatunga sera hiyo mwaka 2016 hakukuwa na mambo ambayo leo yanatokea licha ya kuwa yalikuwepo na hakuna mtu angeweza kufasiri nini kitatokea miaka michache mbele na kwamba wizara inatunga na kusimamia sera, kanuni, miongozo na sheria za utekelezaji wa majukumu.
“Tumekuwa na utaratibu huu tangu tunaanza mchakato wa kukutana na makundi mbalimbali na leo tumeona tukutane na makundi Anuai wenye changamoto mbalimbali za ulemavu lakini ni wadau wetu muhimu katika sera, tunajaribu kuifanyia mapitio,” alisema.