Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo amewakaribisha wawekezaji kutoka Jamhuri ya Latvia kuja nchini kuwekeza katika sekta
mbalimbali ikiwemo sekta ya Kilimo na TEHAMA.

Balozi Dkt. Shelukindo ametoa wito huo wakati, akizungumza na Mkurugenzi Mkuu anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Uwili katika Wizara ya Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Latvia, Nils Jansons aliyemtembelea ofisini kwake jijini Dodoma kwa lengo la kumsalimia na kumpongeza kwa kuteuliwa hivi karibuni.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo akizungumza na Mkurugenzi Mkuu anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Uwili katika Wizara ya Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Latvia, Bw. Nils Jansons alipomtembelea ofisi kwake jijini Dodoma tarehe 10 Machi 2023. Pamoja na mambo mengine Viongozi hao walikubaliana kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Latvia.

Amesema, Tanzania inayo ardhi ya kutosha kwa uwekezaji wa kilimo cha mazao mbalimbali ya chakula na biashara hivyo wawekezaji kutoka Latvia ambayo ni miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri kwenye sekta ya kilimo duniani wanakaribishwa.

“Nimefurahishwa na ziara yako hapa Tanzania. Latvia ni miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri katika sekta ya kilimo duniani. Tunaunga mkono ushirikiano na Tanzania kwenye sekta hiyo na tunawakaribisha wawekezaji wenye tija kuja kuwekeza kwenye sekta mbalimbali hususan kilimo na TEHAMA ” alisema Balozi Dkt. Shelukindo.

Tanzania inayo ardhi ya kutosha kwa uwekezaji wa kilimo cha mazao mbalimbali ya chakula na biashara.

Awali, akizungumza kwenye Majadiliano ya Kwanza ya Kisiasa baina ya Tanzania na Latvia, Balozi Swahiba Mndeme, Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, amesema Tanzania inathamini ushirikiano uliopo baina yake na Latvia.

Amesema, majadiliano hayo ambayo yanalenga kuimarisha ushirikiano baina ya pande mbili, yamekuja wakati muafaka kwa nchi hizi mbili ili kuziwezesha kujiwekea malengo na
mikakati mipya ya kuuimarisha ushirikiano ambao ulikuwa hafifu miaka ya nyuma.

Uapisho: Dkt. Wilson Mahela aapa Ikulu Chamwino
Mila potofu zinaharibu ndoto za walio wengi: Mbunge Tawfiq