Mwimbaji nyota wa kike kutoka nchini Nigeria Tems, amepata fursa ya kushirikishwa kwenye moja ya nyimbo zitakazopatikana kwenye album mpya ya mwanamuziki mkubwa kutoka nchini Marekani ‘Future’, wimbo ambao unamkutanisha Tems na rapa Drake.

“Wait Fo U” ndio jina la wimbo, ambao ndani yake Future amewakutanisha Tems pamoja na Drake ikitajwa kama moja ya wimbo ambao idadi kubwa ya mashabiki wameonyesha shauku ya kutaka kuisikiza punde baada ya orodha ya nyimbo 16 zitakazopatikana kwenye album hiyo ambayo itaachiwa rasmi Aprili 29, 2022.

Mara kadhaa kumekuwa na mijadala kuhusu wasanii wa Nigeria wanavyoweza kuupenyeza muziki wao kwenye soko la dunia, mafanikio yao pamoja na nguvu inayoonekana kujijenga siku baada ya siku.

Hivi karibuni tulitoa habari ya kiwango cha pesa alicholipwa mwanamuziki Wizkid kwaajili ya kutumbuiza kwenye tamasha la Rolling Loud huko nchini Canada kama mmoja wa wasanii muhimu ‘Headliner

Nyota wengine wakubwa walipata nafasi ya kushirikishwa kwenye album hiyo ni pamoja na Young Thug, Kanye West, Kodak Black pamoja na Gunna.

Huu ndio ugonjwa unaomsumbua mke wa Justine Bieber 'Hailey'
Mohamed Hussein: Kilicho mbele yetu ni halali ya Simba SC