Takribani Wajawazito 356,000 walionusurika katika matetemeko ya ardhi lililopoteza maisha ya watu zaidi ya 5,900 nchini Uturuki na Syria wanahitaji kupata huduma za afya ya uzazi kwa dharura huku wengi wao wakillamika kukosa unyumba na huduma muhimu.
Wanawake hao ni pamoja na 226,000 kutoka nchini Uturuki na 130,000 nchini Syria, na kati yao Wanawake 38,800 wanatarajiwa kujifungua mwezi ujao (Machi – 2023).
Wajawazito hao, wengi wamepoteza wapendwa wao, nyumba na mali huku wengi wao wakijihifadhi katika kambi za muda au kuishi katika mazingira ya baridi kali na kukosa chakula, maji safi, na huduma muhimu nyinginezo hivyo kuhatarisha afya zao.
Maelfu ya majengo, ikiwa ni pamoja na hospitali na vituo vinavyoungwa mkono na UNFPA, yameporomoka au kuharibiwa, na hivyo kukata fursa ya wanawake kupata taarifa na huduma za afya ya uzazi na kujamiiana pale wanapozihitaji.