Takribani watu 300 wameaga Dunia, baada ya tetemeko kubwa la ardhi kupiga usiku wa kuamkia leo Septemba 9, 2023 na kuharibu majengo na mali katika Mji wa kale na wa kihistoria wa Marrakesh uliopo nchini Morocco.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo kupitia taarifa yake imeeleza kuwa, tetemeko hilo la ardhi limewaua watu 296 katika majimbo ya na manispaa za Al-Haouz, Marrakesh, Ouarzazate, Azilal, Chichaoua na Taroudant na Watu wengine 153 wamejeruhiwa.

Kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa juu katika Milima ya Atlas, takriban kilomita 70 kusini mwa mji wa Marrakesh huku Vyombo vya Habari vya Morocco vikilitaja tetemeko hilo kuwa lenye nguvu zaidi kuwahi kutokea nchini humo.

Hata hivyo, Mamlaka ya Morocco inayofuatilia matetemeko ya ardhi imelitaja kuwa katika ukubwa wa 7.2 katika kipimo cha Richter wakati mamlaka ya Jiolojia ya Marekani ikisema tetemeko hilo lilikuwa na ukubwa wa 6.8.

Athari za Tetemeko la kina cha kilomita 10. Picha ya Antonio Bronic/Reuters.

Mapema mwaka 2004, takriban watu 628 walifariki na wengine 926 walijeruhiwa wakati tetemeko la ardhi lilipopiga eneo la Al Hoceima kaskazini mashariki mwa Morocco.

Aidha, Tetemeko la ardhi la El Asnam la mwaka 1980 katika nchi jirani ya Algeria, pia lilikuwa mojawapo ya matetemeko makubwa na ya uharibifu zaidi katika historia ya hivi karibuni, liliilowaua watu 2,500 na kuwaacha watu 300,000 bila makaazi.

Ajali ya Basi, Lori yauwa 14, majeruhi hali tete
Mauaji watu 560 yamuibua Rais Museveni