Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini nchini – SGT imesema haijapata taarifa zozote za kutokea kwa madhara kutokana na tetemeko la ardhi lililoyakumba baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Dodoma na Singida.

SGT kupitia taarifa yake kwa umma iliyoitoa hii leo Februari 17, 2023 na kusainiwa na Mtendaji Mkuu imekumbusha kuwa Mikoa ya Singida na Dodoma imepitiwa na ukanda wa bonde la ufa la Afrika Mashari mkondo wa mashariki.

Imesema, “Kutokana na hali hii watu wanakumbushwa kujenga nyumba bora kwa kuzingatia viwango halisi ya ujenzi, kupata ushauri wa kitaalamu wa aina ya majengo yanayofaa na kuepuka kujenga nyumba katika miinuko kama ambavyo taarifa hii inafafanua hapo chini.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Februari 18, 2023
Tuhuma zaibuka mawasiliano washirika wa Rais kudukuliwa