Wadukuzi kutoka nchini Israeli, wanadaiwa kuingilia mawasiliano binafsi ya washirika wawili wa Rais wa Kenya, William Ruto wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka uliopita 2022.

Hatua hiyo imebainika baada ya uchunguzi wa pamoja uliofanywa na wanahabari na ripoti hiyo kuchapishwa katika magazeti ya Haaretz ya nchini Israeli na The Guardian la nchini Uingereza.

Rais wa Kenya, William Ruto. Picha ya La crox.

Ripoti hizo zinasema, mdukuzi huyo aliingia kwenye mawasiliano ya washirika hao kwa lengo la kukusanya taarifa za kiintelejensia kumhusu Ruto, lakini pia kusambaza ujumbe wa kisiasa wa kupotosha dhidi yake.

Waliolengwa katika udukuzi huo, ni Dennis Itumbi na Davis Chirchir ambao ni washauri wa kisiasa wa Ruto na inasemekana mawasiliano yao ya barua pepe na Telegram, yaliingiliwa na mdukuzi aliyefahamika kwa jina la Tal Hanan.

Kiongozi wa Upinzani, Raila Odinga. Picha ya BBC.

Hata hivyo, uchunguzi huo haujabaini ni nani aliyewaajiri wadukuzi hao, lakini kiongozi wa wengi katika bunge la Kenya Kimani Ichung’wa amewashtumu viongozi wa upinzani kutoka muungano wa Azimio la Umoja akiwahusisha na tukio.

Hata hivyo, wapinzani hawajajibu shutuma hizo ingawa Raila Odinga ambaye amekataa kumtambua Ruto kama rais, amekunuliwa akisema muungano huo uliwaajiri wadukuzi kubaini ukweli, kuhusu mshindi wa uchaguzi wa urais akidai yeye ndiye aliyeshinda.

Hakuna taarifa za madhara ya tetemeko la ardhi: SGT
Tetemeko lazua taharuki Dodoma, Singida