Kiungo Nemanja Matic, 27, amemwambia meneja mpya wa Chelsea Antonio Conte, kuwa anataka kuungana na meneja wake wa zamani Jose Mourinho aliyekwenda Manchester United (Sun).

Arsenal wametoa dau la pauni milioni 25 kumtaka winga wa Leicester Riyad Mahrez, 25 (Daily Express).

Arsenal hawana mpango wa kumsajili Mahrez (Dily Mirror)

Wes Morgan, Kasper Schmeichel na Robert Huth wamemtaka mshambuliaji wao Jamie Vardy, 29, kutokwenda Arsenal (Daily Telegraph), lakini Alan Smith ambaye aliwahi kuzichezea timu hizo mbili anaamini Vardy hana budi kwenda Emirates (Talksport).

Leicester wametoa dau la pauni milioni 8 kumtaka kiungo Nampalys Mendy kutoka Nice, wakijiandaa na kuondoka kwa N’Golo Kante (Daily Mail).

Tottenham wana matumaini ya kukamilisha usajili wa mshamuliaji wa AZ Alkmaar, Vincent Jansen, 21, ambaye alikuwa mfungaji bora Uholanzi msimu uliopita (Daily Mirror)

Everton watamwambia beki wa kati John Stones kuwa hawatomuuza, licha ya mchezaji huyo kuwa tayari kulazimisha uhamiso wake (Daily Mirror)

Kiungo wa Roma Radja Nainggolan, 28, amesema ana furahia maisha ya Italia, lakini dau kutoka Chelsea ni “jambo kubwa” na la kuzingatiwa (Gazzetta dello Sport)

Kiungo wa Newcastle Moussa Sissoko, 26, amesema anataka kuondoka, baada ya timu kushuka daraja na kuwa Arsenalni “klabu yake ya moyoni” (Foot Mercato).

Paris St-Germain watamtangaza meneja wa Sevilla Unai Emery kuwa meneja mpya, kuchukua nafasi ya Laurent Blanc (Marca).

Beki wa PSG Marquinhos, 22, ambaye amehusishwa na kwenda Chelsea na Manchester United, amesema anafanya mazungumzo kuhusu hatma yake na mabingwa hao wa Ufaransa (Daily Express).

Middlesbrough wamekataa nafasi ya kumsajili beki wa kati wa Liverpool Martin Skirtel, ambaye sasa atakwenda Besitkas (Northern Echo).

Meneja wa Aston Villa Roberto di Matteo anataka kumsajili mshambuliaji wa Crystal Palace (Birmingham Mail).

Video: Waziri Mpango Ametuletea Mpango wa Maendeleo wa Taifa2016/17, Kayataja Mambo Haya
Wasifu Wa Stephen Okechukwu Keshi