Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imezifutia usajili dawa mbalimbali za kutibu magonjwa ya binadamu na kuziondoa kwenye soko pamoja na kusitisha matumizi yake kutokana na kuwa na madhara makubwa kwa wagonjwa.
Hayo yamesemwa Jijini Arusha na Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo, alipokuwa akifungua mafunzo ya siku tano ya wakufunzi wa ufuatiliaji juu ya ufundishaji na uhamasishaji wa masuala ya udhibiti wa madhara yatokanayo na matumizi ya dawa zisizo salama.
Amesema kuwa katika kudhibiti matumizi ya dawa zisizofaa TFDA imeondoa dawa ya sindano aina ya Chloramphenical kwenye soko baada ya shirika la Afya Duniani WHO, kubaini dawa hiyo ina madhara kwa watumiaji, pia mamlaka hiyo imefuta usajili wa dawa zingine kama vile Ketoconazole, (vidonge) Phenylpropanalamine, Dextropropoxyphene, Nimesulide,stavudine 40, Gatifloxacin, Rofecoxib, pamoja na Celecoxib baada ya kuthibitika zina madhara kwa watumiaji.
Aidha, Mkurugenzi huyo wa TFDA amesema kuwa mafunzo hayo yanashirikisha wakufunzi 60 nchini kote na yanafanyika katika mikoa mbalimbali yakiwashirikisha Madaktari, Manesi, na wafamasia walioko kwenye hospitali, vituo vya afya na Zahanati.
-
Nchemba: Wapinzani hawakupaswa kusimamisha wagombea
-
Majaliwa apiga marufuku Mawaziri kutoa matamko
-
Idadi ya walifariki kwa mlipuko Kagera yaongezeka
Hata hivyo, ameongeza kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuongeza idadi ya wakufunzi wa masuala ya usalama wa dawa kutoka 73 hadi 133 na tayari katika kipindi cha miaka mitatu 2014/ 15 hadi 2017/18, Mamlaka ya chakula na dawa imehamasisha watendaji wa afya wapatao 2000 nchini kote na sasa uhamasishaji unaendelea katika mkoa wa Katavi.