Klabu ya Crystal Palace inajipanga kuongeza dau ili kufanikisha azma ya kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Ubelgiji na klabu ya Liverpool, Christian Benteke.

Gazeti la Daily Mail, limeripoti kwamba The Eagles tayari wameshawasilisha ofa ya Pauni milioni 25, lakini uongozi wa Liverpool uliiweka kapuni kwa kigezo cha kutokua na thamani na mshambuliaji huyo ambaye hayupo kwenye mipango ya Jurgen Klopp kwa msimu ujao wa ligi.

Kutokana na suala hilo viongozi wa Crystal Palace wanajipanga kuwasilisha ofa nyingine ya Pauni milion 30 kwa kuamini watafanikisha mpango wao wa kumsajili Benteke.

Benteke alisajiliwa na klabu ya Liverpool kwa ada ya uhamisho ya Pauni milion 32.5 akitokea Aston Villa mwanzoni mwa msimu uliopita.

Arsenal, Chelsea Zamuwania Romelu Lukaku
Watzke: Tulistahili Kumuachia Mkhitaryan Aende Old Trafford