Kikosi cha Liverpool kitashuka dimbani kukabiliana na Southampton mwishoni mwa juma hili, bila ya kuwa na kiungo mshambuliaji Adam Lallana.

Lallana mwenye umri wa miaka 28, alipatwa na majeraha nyonga wakati wa mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya timu yake ya taifa ya England dhidi ya mabingwa wa soka duniani mwaka 2010, timu ya taifa ya Hispania uliomalizika kwa sare ya mabao mawili kwa mawili.

Kiungo huyo alilazimika kufanyiwa vipimo aliporejea Anfield jana mchana na ilibainika hatoweza kucheza mchezo wa siku ya jumamosi ambao utaunguruma kwenye uwanja wa St Mary’s Stadium.

Hata hivyo kabla ya kuruhusiwa kuondoka kwenye kambi ya timu ya taifa ya England, Lallana alifanyiwa vipimo vya awali na majibu yake yalionyesha aliumia kwa kiasi kikubwa na ilishauriwa apumzishwe kwa muda wa majuma kadhaa.

Mayweather amtembelea Trump
Santi Cazorla Kuikosa Man Utd