Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Gabriel Migire amesema kuwa mabasi yote ya abiria nchini yataanza kutumia mfumo wa kukata tiketi kwa njia ya kielektroniki kuanzia Julai mosi mwaka huu.
Katibu Mkuu Migire ametoa maelekezo hayo jijini Dodoma na ambapo amesema kuwa majaribio ya mfumo huo yataanza Aprili Mosi na kuendelea hadi Julai mosi.
Amewataka wadau wote wa usafirishaji na abiria kutumia kipindi hicho cha majaribio kutoa kupata elimu ya matumizi ya tiketi za kieletroniki na kwamba tayari ujenzi wa mfumo wa ukataji tiketi kwa mtandao umekamilika na upo tayari kwa matumizi.
Aisha amesema Wizara kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Ardhini LATRA, Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA na Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA) wamejipanga kutoa elimu kwa umma kuhusu matumizi ya tiketi hizo za kielektroniki.