Jeshi la Polisi nchini Nigeria, limeimarisha usalama baada ya Marekani kuziamuru familia za wanadiplomasia wake kuondoka katika mji mkuu wa Abuja, kutokana na vitisho vya mashambulizi ya kigaidi.
Licha ya ufinyu wa taarifa za vitisho hivyo, wakazi wa Abuja wamekuwa na wasiwasi kufuatia balozi za kigeni kubadilisha taratibu zao za usafiri, zikidai kiwango cha tetesi za uwepo wa mashambulizi ya kigaidi kimeongezeka.
Vikosi vya Nigeria, vinapambana na wapiganaji wa kijihadi katika maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo, na wanamgambo wenye mafungamano na kundi la Dola ya Kiislamu wamekiri kuhusika na mashambulizi kadhaa.
Hata hivyo, Polisi wa Nigeria imewapanga makamanda wa vitengo vya kimkakati ili kuimarisha usalama katika maeneo yao, huku Marekani ikionya juu ya uwezekano wa shambulio jingine siku ya Jumamosi (Oktoba 29, 2022 jijini Johannesburg, nchini Afrika ya Kusini.