Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump amefurahia hatua ya kampuni ya Twitter kununuliwa na bilionea Elon Musk, akisema kampuni hiyo maarufu ya mtandao wa kijamii hivi sasa ipo mikononi mwa mtu mwenye akili timamu. 

Musk amekamilisha ununuzi wa kampuni hiyo Oktoba 27, 2022 kwa malipo ya dola bilioni 44, baada ya miezi kadhaa ya tetesi na minong’ono juu ya kufanyika kwa biashara hiyo. 

Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump. Picha: US Today

Kupitia mtandao wake mwenyewe, ujulikanao kama Truth Social, Trump ametumia maneno makali, akisema “Ninafurahi sana kuwa Twitter haitaendeshwa na wendawazimu wenye sera za mrengo wa kushoto.” 

Hatua ya Elon Musk, kuimiliki Twitter imesababisha hofu miongoni mwa wanaharakati kuwa itageuzwa jukwaa la unyanyasaji na habari za kupotosha, kwa hoja kwamba Musk mwenyewe anajulikana kwa kuwashambulia watumiaji wa mtandao huo. 

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Octoba 29, 2022     
Tishio la ugaidi: Polisi yaimarisha usalama