Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imekusanya sh.trilioni 7.27 katika kipindi cha miezi sita ya mwaka wa fedha kuanzia Julai hadi Desemba mwaka jana.

Ambapo kiasi hicho ni ongezeko la asilimia 12.74 kilichokusanywa ukilinganisha na makusanyo ya sh. trilioni 6.44 yaliyokusanywa katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2015/16.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Richard Kayombo, alipokuwa akitoa takwimu za makusanyo hayo jijini Dar es salaam mbele ya waandishi wa habari, kuhusu makusanyo ya kodi katika kipindi cha nusu mwaka wa fedha 2016/17.

Kayombo amesema kuwa makusanyo ya Julai 2016 yalikuwa sh.trilioni 1.069, Agosti sh.trilioni 1.154, Septemba sh.trilioni 1.378, Oktoba sh.1.131, Novemba sh.trilioni1.123 na Desemba sh.trilioni1.414.

Mbowe: Chadema tunachezewa rafu za kisiasa
CCM haimuachii Lowassa, Polepole aanza nae...