Rais wa Marekani Donald Trump amekubali kuanza mchakato wa kumkabidhi madaraka Rais mteule wa Marekani Joe Biden ikiwa ni zaidi ya wiki mbili baada ya kutangazwa kuwa mshindi.
Rais Trump amekiri muda umefika na kulitaka shirika linaloshughulikia mabadilishano ya madaraka lifanye kile kinachostahili kufanywa na kuiasa timu yake kutoa ushirikiano katika mchakato huo.
Wakati hayo yakiendelea timu ya Biden, imefurahishwa na kuanza kwa mchakato huo huku Rais mteule anajiandaa na sherehe za kuapishwa Januari 20, 2021.
Uamuzi wa leo kwa wanademocrat ni hatua iliyohitajika kuanza kukabiliana na changamoto zinazokumba taifa hilo, ikiwemo kudhibiti ugonjwa wa virusi vya corona na kuboresha uchumi tena.
Sambamba na hayo yote, ofisi ya utawala wa huduma za serikali imesema inamtambua Bwana Biden kama “mshindi”.