Rais wa Marekani, Donald Trump ameapa kuiangamiza Korea Kaskazini endapo itaendelea na mpango wake wa kufanya majaribio ya silaha za nyuklia na makombora ya masafa marefu.
Ameyasema hayo mara baada ya Ikulu ya nchi hiyo kutoa ratiba ya ziara ya Rais huyo katika mataifa matano barani Asia mwezi Novemba ili kushiriki katika mikutano ya ukanda huo ya kujadili mambo mbalimbali.
Aidha, Ikulu ya Marekani imezitaja nchi ambazo Rais Trump atazitembelea ndani ya siku kumi na moja za ziara yake barani humo kuwa ni pamoja na washirika wake wakubwa ambao ni Japan, China, Korea Kusini, Vietnam, Ufilipino na Hawaii.
Ziara hiyo ya Rais, Trump inatarajiwa kuimarisha harakati zake za kimataifa za kukabiliana na tishio la Korea Kaskazini ambayo amekuwa akiipinga kuhusiana na mpango wake wa silaha za nyuklia.
-
Mmiliki wa Facebook ‘atifuana’ na Trump
-
Kenyatta amtolea uvivu Raila, amtaka ajiengue au
-
Video: 50 Cent aeleza alivyokataa pesa za Trump
Hata hivyo, Korea Kaskazini na Marekani zimekuwa zikirushiana maneno ambayo yamesababisha mvutano mkali kati kuhusiana na majaribio mbalimbali ya silaha za nyuklia yanayofanywa na Korea Kaskazini katika miezi ya hivi karibuni