Rais wa Marekani, Donald Trump amezionya nchi za Korea ya Kaskazini na Iran kufuatia vitisho vinavyotolewa na nchi hizo vya kufanya majaribio mbalimbali ya silaha za nyuklia, huku akisema kuwa atazigeuza mavumbi kama ikibidi.

Ameyasema hayo katika hotuba yake aliyoitoa katika mkutano wa Baraza la Umoja wa Mataifa unaoendelea Jijini New York, ambapo amesema kuwa silaha za nyuklia ni tishio kwa usalama wa dunia.

Aidha, Katika hotuba yake hiyo ya kwanza katika mkutano wa Baraza la Umoja huo unaofanyika Jijini New York, Trump ameonya kuwa Marekani itaiangamiza Korea kaskazini iwapo italazimika kujitetea ama kuwalinda washirika wake.

Hata hivyo, katika hatua nyingine Trump amesema kuwa Iran ni nchi ya kifisadi inayoongozwa kidikteta, hivyo ameitaka kuacha mara moja kusaidia makundi ya kigaidi ambayo yamekuwa yakihatarisha amani ya mashariki ya kati.

 

Video: Polisi Dar yakamata 'Wasiojulikana' watano
Jaji Mkuu Kenya azungumzia vitisho vinavyomkabili kwa kufuta uchaguzi