Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limetangaza kuwakamata watu watano ambao wamekiri kufanya uhalifu na kuvunja katika ofisi ya Mawakili ya Prime Atorneys iliyopo katika jengo la Prime house, Mtaa wa Tambaza, Upanga jijini Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa ambapo amesema kuwa jeshi la polisi limeweza kuwakamata watu hao ambao mwanzo baadhi ya wananchi walikuwa wakisema watu wasiojulikana ambao walifanya uhalifu huo na kudai wamekiri kuhusika na uvunjaji wa ofisi hiyo na kuiba.

“Kutokana na msako mkali jeshi la polisi limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watano kuhusiana na kesi ya uvunjaji wa ofisi ya Mawakili ya Prime Atorneys mnamo Septemba 12, 2017 jeshi la polisi lilipokea taarifa ya kuvunjwa kwa ofisi ya mawakili hao ambapo wahalifu hao walifanikiwa kuvunja na kuiba kasiki iliyokuwa na pesa milioni tatu laki saba, waliiba kompyuta mpakato mbili pamoja na nyaraka mbalimbali za ofisi hiyo na wateja,”amesema Kamanda Mambosasa

Magazeti ya Tanzania leo Septemba 20, 2017
Trump: Tutaigeuza mavumbi Korea Kaskazini