Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba SC Salim Abdallah ‘Try Again’ amewatuliza mashabiki wa Simba SC wanaoendelea kuhoji nafasi ya Kocha Juma Mgunda, baada ya kutambulishwa kwa kocha Msaidizi Ouanane Sellami.

Simba SC ilimtangaza Ouanane Sellami jana Alhamis (Januari 19) majira ya jioni, ambaye anaungana na makocha wengine klabuni hapo kwa ajili ya kuongeza ujuzi wa kukinoa kikosi cha Msimbazi.

Try Again ametumia ukurasa wake wa Twitter kutuliza sintofahamu hiyo kwa mashabiki, akisisitiza kuwa hakuna kocha yoyote atakayeondoka klabuni hapo, baada ya kutambulishwa kwa Kocha Msaidizi Ouanane.

“Makocha wote waliokuwepo wataendelea kuwepo, tumeongeza nguvu”. ameandika Try Again
Hata hivyo inaelezwa kuwa ujio wa Kocha Ouanane Sellami ni pendekezo la Kocha Mkuu Robertinho ambaye tayari ameshaanza kazi ya kukinoa kikosi cha Simba SC.

Juma Mgunda alifanya kazi kama Kaimu Kocha Mkuu wa Simba SC tangu Septemba 2022, baada ya kuondoka kwa Kocha kutoka Serbia Zoran Maki.

Rais avunja Bunge na kuitisha uchaguzi
78 wafariki majira ya baridi kali