Tukio la kupatwa kwa mwezi lisilokuwa la kawaida linatarajiwa kutokea hii leo tarehe 27/7/ 2018 na inasemekana kuwa litachukua muda mrefu zaidi katika karne ya 21, kulingana na taarifa iliyotolewa na shirika la usimamizi wa anga (NASA).

Kupatwa kwa mwezi hutokea wakati Jua, Dunia na Mwezi zinapokua kwenye mstari mmoja, hii inamaanisha kwamba dunia iko katikati ya jua na mwezi hatua inayoziba mwanga wa jua.

Aidha, Katika awamu tofauti tofauti kupatwa huko kwa mwezi kutafanyika kwa muda wa saa tatu na dakika 55, ambapo kutaonekana Ulaya, Afrika, Mashariki ya Kati , katikati mwa Asia na Australia ikiwa ni maeneo yote isipokuwa Amerika ya Kaskazini.

Kwa mujibu wa shirika la anga (NASA) eneo ambalo tukio hilo litaonekana vizuri ni pamoja na Afrika Mshariki, Mashariki ya Kati na katikati mwa bara Asia.

Hata hivyo, tukio hilo halitaonekana katika maeneo ya Amerika ya Kaskazini, ambapo Amerika ya Kusini unaweza ukaonekana katika miji ya Buenos Aires, Montevideo, Sao Paulo na Rio de Janeiro.

 

Fabian Schar kuimarisha ukuta Newcastle United
Leicester City wabuni mkakati wa kumzuia Harry Maguire