Waziri wa Nishati, Januari Makamba amesema Serikali imekusudia kujenga Chuo (Polytechnic), cha mambo ya Mafuta, Gesi na Umeme Mkoani Lindi, ili kuwajengea Wazawa uwezo juu ya nishati hiyo muhimu kwa uchumi wa Taifa.

Makamba ameyasema hayo mara baada ya uwekaji wa saini ya mkataba wa uzalishaji na ugawanaji mapato (PSA), kitalu cha Ruvuma – Mtwara na kuongeza kuwa Tanzania pia itaanza kuingia kwenye uchumi wa gesi kutokana na jitihada thabiti za Serikali.

Waziri wa Nishati, Januari Makamba. (Mwenye tai Nyekundu)

Amesema, “Kule Arusha, tupo kwenye hatua za mwisho za majadiliano kwenye ule mradi wetu wa kuchakata gesi utakao gharimu zaidi ya trilioni 70. Huu utakuwa uwekezaji mkubwa barani Afrika.”

Aidha Waziri Makamba ameongeza kuwa, “Lakini pia tutajenga Special Economic Zone ndani ya eneo la mradi ili kuchochea maendeleo ya Lindi na Mtwara baada ya mradi kukamilika.

Mwili wa aliyefukiwa na kifusi wapatikana
Raia watakiwa kujihami kwa chakula na maji