Hatimaye timu ya Taifa ya Wanawake ya mpira wa miguu nchini “Twiga Stars”  ambayo imekuwa ikifanya vibaya kila kukicha katika mashindano yake inayoshirikii  mapema leo Aprili Mosi imeweka wazi kuwa ni bora timu hiyo iwe mikononi mwa Serikali kuliko ilivyo sasa kuwa mikononi mwa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF).

Akiuzungumza mbele ya waandishi wa Habari katika tukio lililowakutanisha Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura pamoja na Wachezaji w kikosi cha timu hiyo ya Taifa ya Wanawake, Twiga Stars, Meneja wa Timu hiyo, Bi. Furaha Francis amebainisha kuwa  wamekuwa wakitembelea nchi mbalimbali kimichezo ambapo wamekuta timu hizo za Wanawake zipo mikononi mwa Serikali na wamekuwa wakifanya vizuri tofauti na wao.

“Mhe. Waziri.  Tunaomba sana huko kote tulikozunguka kimichezo na timu yetu, tumweza kukuta maofisa wa Serikali wakigharamia timu zao pamoja na kuzishughulikia na wanafanya vizuri hivyo tunaomba muliangalie hili” alieleza Meneja huyo na kuongeza kuwa endapo watakuwa chini ya Serikali wataweza kufanya vizuri zaidi kwani wataitumikia ipasavyo kuliko sasa wamekuwa kama hawana mtu wa kuwaendesha.

Kwa kauli hiyo, Meneja huyo amebainisha kuwa, timu nyingi za wanawake zipo mikononi mwa Serikali na zimekuwa zikifanya vizuri tofauti na zinazosimamiwa na watu wengine hivyo kauli yake hiyo amebainisha kuwa TFF imeshindwa kuendeleza ligi hiyo na hata mipango thabiti ya kimaendeleo imeshindwa kufikia malengo.

Kwa upande wao wachezaji wa timu hiyo akiwemo Kapteni wa timu hiyo, Asha Rashid, aliomba Serikali kuangalia uwezekano wa kuwasaidia  kutimiza ndoto zao kwani  kwa namna walivyojitoa kuitumikia Tanzania katika michezo  ni kwa miyo yaao hivyo ilikuwapa wachezaji wengi zaidi ni pamoja na kuanzisha ligi ya wanawake na kuibua vipaji zaidi hasa  kwa watoto wadogo waliopo mashuleni.

Aidha, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura  amewapongeza wachezaji hao na kuwataka wasivunjike moyo kwa sasa kwani Serikali ipo nao bega kwa bega katika kutimiza malengo yao ya kila siku.

Ambapo amewataka wachezaji hao kuwa mfano mzuri kwa jamii na wasichana wengine wawaone wao kama kioo na kipimo katika kufikia malengo ya mpira wa miguu kwa wanawake. Pia amewagusia kwa wawapo kwenye jamii kuepuka mambo mabaya na baadala yake wafanye kazi na kuendeleza mazoezi ya kila siku.

 

b8Mjumbe wa Kamati ya Utendaji na Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Wanawake TFF, Amina Karuma (Kulia)  akitoa kilio chake kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura (aliyekaa katikati) juu ya timu yao hiyo ya Taifa ya Twiga Stars kushindwa kufanya vizuri kutokana na kutokuwa na mipango endelevu ikiwemo suala la ligi Kuu ya Wanawake hapa nchini.

DSC_8851Baadhi ya wachezaji wa Twiga Stars wakifuatilia mkutano huo na Naibu Waziri wa Michezo (Hayupo pichani).

DSC_8844Golikipa wa timu ya Twiga Stars akitoa shukrani zake kwa Naibu Waziri…

DSC_8858Baadhi ya wachezaji wa Twiga Stars wakifuatilia  mkutano huo..

DSC_8850Meneja wa Timu ya Twiga Stars, Bi. Furaha Francis akizungumza mbele ya wanahabari wakati akimuelezea Naibu Waziri wa Michezo (hayupo pichani) juu ya Twiga Stars ni bora kuwa mikononi mwa Serikali.

DSC_8855Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura (katikati) akizungumza na wachezaji wa timu ya Twiga Stars (hawapo pichani) wakati wa mkutano huo aliokutana nao mapema leo Aprili 1.2016, jijini Dar es Salaam.

Aston Villa Wamshimamisha Gabriel Agbonlahor
Serengeti Boys Kupapatuana Na The Pharaohs Kesho