Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Zahara Michuzi ameipongeza Kampuni ya Geita Gold Mining Limited – GGML, kwa kuanzisha program zinazolenga kufungua fursa mbalimbali zinazowainua wanawake kielimu, kijamii na kiuchumi.
Michuzi ametoa kauli hiyo hivi karibuni Mjini Geita, katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani na kuongeza kuwa GGML na Halmashauri hiyo wamekuwa wakishirikiana katika program za kuwajengea uwezo wasichana kupitia shule wanazosoma ikiwemo Shule ya Wasichana Nyankumbu iliyopo mkoani Geita.
“GGML inaunga mkono Serikali kutoa huduma bila kuwa na vikwazo vya kibajeti. Kwa hiyo ushirikiano unahitajika na sisi tulioaminiwa kwa niaba ya serikali tuhakikisha lengo na azma ya serikali ya kutatua changamoto za wananchi linafikiwa,” alisema Michuzi.
Aidha, ameipongeza kampuni hiyo kwa kuendelea kujali wananchi wanaozunguka mgodi huo kupitia mpango wa uwajibika wa kampuni kwa jamii (CSR) pamoja na kutekelezwa matakwa ya sheria madini kiasi cha kuwa mshindi zaidi ya mara mbili katika tuzo za mlipa kodi mkubwa wa sekta ya madini.
Elimu ya mafunzo na ufundi stadi: Majaliwa aipongeza GGML
GGML, imekuwa ikitekeleza program mbalimbali za kuwainua wanawake ikiwamo program ya Female Future Tanzania Programme (FFT) ambayo inaratibiwa na Chama cha Waajiriwa Tanzania (ATE) kwa lengo la kuwajengea uwezo wanawake kushika nyadhifa za juu.
Pia kampuni hiyo ambayo hutoa kipaumbele cha ajira kwa wanawake, inatekeleza program ya masomo ya shahada ya uzamili katika usimamizi wa biashara (MBA) pamoja na program nyingine za mafunzo ndani ya kampuni kwa lengo la kuwainua wanawake kushika nafasi za juu za uongozi.