Baada ya kuambulia visago viwili mfululizo kutoka kwa Simba SC ya Tanzania, Uongozi wa mabingwa wa Soka nchini Uganda Vipers SC umemtimua kocha wao Roberto Luiz Bianchi Pelliser ‘Beto Bianchi’.

Maamuzi ya kumtimua kocha huyo yemkuja baada ya kikosi cha Vipers SC kuwasili nchini Uganda kikitokea Tanzania, ambako kilicheza mchezo wa Mzunguuko wanne wa Kundi C, ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Simba SC na kupoteza kwa kufungwa 1-0.

Kocha huyo aliyeajiriwa klabuni hapo mwezi Januari 2023, baada ya kuondoka kwa Kocha Robertinho aliyeibukia Simba SC ya Tanzania, amekuwa na wakati mgumu wa kupata matokeo yaushindi tangu alipoanza kazi yake klabuni hapo.

Taarifa ya Vipers SC ya kumtimua kocha huyo imeeleza: “Vipers Sports Club inatangaza kwamba kandarasi ya Kocha mkuu Beto Bianchi imesitishwa mara moja.

“Klabu ingependa kumshukuru Bianchi kwa juhudi zake wakati alipokuwa klabuni na kumtakia mafanikio katika juhudi zake za baadaye,”

Bianchi anaondoka katika klabu hiyo baada ya kukiongoza kikosi cha Vipers SC katika michezo saba lakini alishindwa kupata ushindi hata mmoja, huku timu hiyo ikishindwa kufunga bao lolote alipoajiriwa Januari 10, 2023.

Jukumu lake kubwa lilikuwa kuiongoza Vipers SC kutinga Hatua ya Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, lakini ameshindwa.

Upande wa Ligi Kuu ya Uganda, Vipers SC inashika nafasi ya nne katika msimamo ikiwa na alama 28, ikicheza michezo 14 nyuma ya KCCA FC na BUL FC.

Bianchi anaungana na makocha wengine wa kigeni ambao wameifundisha Vipers SC hadi sasa akitanguliwa na Roberto Oliviera, Javier Martinez, na Miguel Duarte Da Costa.

Uanzishaji program za fursa: Mkurugenzi Geita aipongeza GGML
Tanzania yafungua ofisi za ubalozi nchini Namibia