Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe amezindua kichwa kimoja cha treni kati ya saba vilivyokuwa vinakarabatiwa katika karakana ya Shirika la Reli Tanzania (TRC), ambao umegharimu Shilingi Bilioni 15 za Kitanzania.

Akizungumza jijini Dodoma wakati akizindua kichwa cha treni ya reli ya kati amesema kipande cha Dar es Salaam-Morogoro chenye urefu wa kilomita 300 na Morogoro-Makutupora-Singida chenye urefu wa kilomita 422 vinaendelea kujengwa.

Vipande hivyo vya reli ya kisasa vyenye urefu wa Kilomita 722, vinajengwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 7.1 na tayari serikali imeshasaini mikataba miwili kwa ajili ya ununuzi wa vichwa vya treni na mabehewa vitakavyoendeshwa kwa umeme.

Waziri Kamwelwe amesema serikali inatarajia kupokea mabehewa ya reli ya kisasa Februari 2021, ambapo pia kipande cha reli hiyo kutoka Dar es Salaam-Morogoro kitakuwa kimekamilika.

Ujenzi wa VETA Kagera wakutana na kizingiti hiki
Chagueni madiwani wa CHADEMA- Lissu