Maelfu ya Ngamia kusini mwa Australia watauawa kwa risasi kutoka kwenye helikopta kutokana na kuwepo kwa joto kali na ukame.

Imeelezwa kuwa kutokana na hali ya ukame ngamia wamekuwa tishio kwenye jamii hivyo unahitajika udhibiti wa haraka. Zoezi hilo la siku tano limeanza Jumatano.

Jamii zinazoishi karibu na makazi ya ngamia hao wamesema wamekuwa wakiishi katika mazingira magumu, kwa sababu ngamia hubomoa uzio, huzunguka nyumba wakijaribu kupata maji kupitia maji yanayodondoka kutoka kwenye viyoyozi.

Joto kali na ukame vimesababisha moto wa nyika nchini Australia kwa kipindi cha miezi kadhaa, lakini hali ya ukame ya nchi hiyo imekuwepo kwa miaka kadhaa.

Ngamia hawana asili ya Australia, walipelekwa nchini humo na walowezi kutoka India, Afghanistan na mashariki ya kati katika karne ya 19.

Man Walter atoa majibu kisa cha Alikiba kuchelewa kuachia ngoma zake
Man Walter aanika madeni anayomdai Alikiba

Comments

comments