Umoja wa Ulaya umeipatia Tanzania jumla ya Euro Million 50 ambazo ni sawa na shilingi Bilioni 130 za kitanzania katika kufadhili Mpango wa Taifa wa umeme vijijini ambapo jumla ya vijiji elfu 12 vitapatiwa umeme.
Hayo yamesemwa hii leo jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dotto James wakati wa utiaji saini juu ya ufadhili huo wenye masharti nafuu ambapo Tanzania haitatakiwa kurejesha Fedha hizo, huku umoja wa Ulaya unalenga kuona mpango wa maendeleo wa taifa wa miaka 5 unafikiwa kikamilifu hususani katika sekta ya nishati katika uzalishaji na usambazaji ili kurahisisha shughuli za kimaendeleo na kupunguza umasikini vijijini.
Aidha, kwa upande wake Kamishna wa Umoja wa Ulaya, Neven Mimica anasema kuwa kufikiwa kwa mpango wa tatu wa umeme vijini REA unaomalizika 2020 kunategemea upatikanaji umeme wa uhakika suala ambalo litachochea kwa kiasi kikubwa kufikiwa kwa mpango wa maendeleo endelevu ya dunia ya mwaka 2025.
Hata hivyo, Ufadhili wa maendeleo ya umoja wa Ulaya kwa Tanzania kwa sasa unafikia jumla ya Trillion I .07