Wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa, wameyataka mataifa ya Morocco na Hispania kuhakikisha uchunguzi huru unafanyika na hatua kuchukuliwa kwa wale waliohusika na vifo vya waafrika 23 waliokuwa wakijaribu kuvuka mpaka wa Melilla, unaotenganisha nchi hizo mbili wakitaka kwenda ulaya.

Taarifa iliyotolewa hii leo Julai 1119, 2022 kutoka Geneva Uswisi na wataalamu watatu wa Umoja wa Mataifa wa mfumo huru wa Kimataifa (IIEM), Justice Yvonne Mokgoro, Dkt. Tracie Keesee na Profesa Juan Mendez imesema, vifo hivyo vilitokea wakati ambapo takribani watu 2000 walijaribu kuvuka uzio mrefu huko kaskazini mwa Afrika.

“Matumizi yoyote ya nguvu yanayotumiwa na maafisa wa Polisi yanapaswa pia kuongozwa na kutekeleza sheria na kanuni za uhalali, tahadhari, umuhimu, uwiano, uwajibikaji na bila ubaguzi,” walisema wataalamu hao.

Waafrika waliokuwa wakijaribu kuvuka mpaka wa Mellila kwa kuruka uzio.

Wataalamu hao, waliopewa jukumu la kuhakikisha wanaangalia masuala ya mamlaka kuendeleza haki na usawa bila ubaguzi wa rangi wakati wa utekelezaji wa sheria na pia wataalamu hawa ni kikosi Kazi cha Wataalam wa Umoja wa Mataifa kuhusu watu wenye asili ya Kiafrika.

IIEM imekusanya taarifa ya tukio hilo kutoka kwa serikali za Hispania na Morocco hususan kuhusu maendeleo ya uchunguzi unaoendelea na imesema “Tutaendelea kufuatilia na kushirikiana na mamlaka za Hispania na Morocco. Tuko tayari kutoa mwongozo na mapendekezo kwa Mataifa na wadau wote husika ili kuhakikisha waathiriwa na familia zao wanapata haki.”

Wataalamu hao wamezitaka serikali zote mbili kutoa taarifa juu ya udhibiti wa ndani wa matumizi ya nguvu na hatua zinazochukuliwa ili kuhakikisha tukio kama hilo halijirudii tena.

Waafrika waliofanikiwa kuvuka mpaka wa Mellila kwa kuruka uzio.

“Tunatambua kuwa uchunguzi umeshaanza na tunatoa wito kwa Hispania na Morocco kuchukua hatua zote muhimu kwakushirikiana na Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika ili kuhakikisha kuna uwajibikaji wa haraka, kuwalipa fidia waathirika na kuzuia tukio la namna hii la vifo likitokea.” Wameongeza wataalamu hao.

Wamesema, watafanya tathmini ya sheria na taratibu za utekelezaji wake katika nchi zote mbili kinyume na viwango vinavyotumika vya haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na Kanuni za Msingi za Umoja wa Mataifa kuhusu Matumizi ya Nguvu na Silaha za moto kwa wasimamizi wa sheria, pia wataangalia mwongozo juu ya silaha zisizo na hatari.

Mbunge arejesha furaha ya Wanafunzi ajali ya moto
UNFPA yawaonesha MSD umuhimu wa 'kila ujauzito'