Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA-Zanzibar), wamesaini mkataba wa mradi kuwajengea uwezo waandishi wa habari, kuandika habari za kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Mradi huo wa miezi mitatu wenye thamani ya dola za Marekani 17,000, umesainiwa kati ya Mkurugenzi wa TAMWA Zanzibar, Dkt. Mzuri Issa Ali na Mwakilishi Mkazi wa UNESCO Tanzania, Michael Toto katika hafla iliyofanyika Tunguu Wilaya ya kati Unguja.

Mkurugenzi wa TAMWA-ZNZ, Dkt. Mzuri Issa (kushoto), akikabadilishana hati ya makaubaliano na mwakilishi mkazi wa UNESCO Tanzania, Michel Toto Tunguu Wilaya ya kati Unguja.

Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt. Mzuri alisema mradi huo utaongeza nguvu mapambano dhidi ya ukatili na udhalilishaji wa wanawake na watoto ambayo ni moja ya mikakati inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya nane chini ya uongozi wa Rais, Dk. Hussein Ali Mwinyi.

Aidha, ameahidi kutekeleza mradi huo kwa kiwango ili kukidhi matarajio ya UNESCO na kwamba wanatumai mradi huo utaleta tija kwa kwa maslahi ya Taifa huku Mwakilishi mkaazi wa UNESCO Tanzania, Michel Toto, akisema mradi huo utawajengea uwezo wanahabari kuondoa mila potofu.

Gharama bidhaa za vyakula kupungua mwezi Mkutukufu
Uturuki kuondoa mabaki ya majengo eneo la tetemeko