Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Husein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea kuweka jitihada za kupunguza gharama za bidhaa za vyakula, katika kipindi cha kuelekea mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Rais Mwinyi, ameyasema hayo hii leo Februari 17, 2023 baada ya sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Msikiti wa Forodhani Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Rais Dkt. Mwinyi Mwinyi akiongea baada ya sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Msikiti wa Forodhani Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Amesema, Serikali itaendelea kuweka mipango madhubuti itakayowezesha kupunguza gharama za bei za vyakula ambapo pia amehahidi kuchangia shilingi milioni tano kukarabati msikiti wa Forodhani.

Februari 12, 2023, Rais Dkt. Mwinyi alifanya ziara ya kushtukiza kwa wafanyabiashara mbalimbali wa maduka ya vyakula ya rejareja, kujionea hali ya chakula ilivyo na bei zake katika eneo la Chake Chake Pemba.

Tetemeko lazua taharuki Dodoma, Singida
UNESCO, TAMWA kuwa ngao ya wanawake na watoto