Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo kuhusu uwekezaji na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kilimo kutoka nchini China, Longping Agriscience – LTD, Liang Shi, Ikulu Jijini Dar es salaam.

Katika mazungumzo hayo ya hii leo Februari 17, 2023 Dkt. Mpango ameipongeza kampuni hiyo kwa nia yake ya dhati ya kuwekeza katika kilimo nchini kwa kutambua uhusiano wa muda mrefu baina ya Tanzania na China.

Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango akifanya mazungumzo na viongozi wa Kampuni ya Longping Agriscience LTD wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Liang Shi, mazungumzo yaliofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam leo Februari 17, 2023.

Amesema, Tanzania inaendelea na jitihada za kuimarisha sekta ya kilimo ikiwemo kuanzisha
programu ya kilimo biashara, yenye lengo la kuwasaidia vijana kushiriki katika sekta hiyo kikamilifu na kuchochochea ukuaji wake kufikia lengo la asilimia 10 ifikapo mwaka 2030.

Aidha, amewasisitiza kutumia ubunifu, utafiti, ulinzi wa mimea na matumizi ya teknolojia rafiki ili kuongeza uzalishaji. Pia kutoa mafunzo na vitendea kazi kwa wakulima na kutumia vema ardhi watakayopata kwa maendeleo endelevu.

Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kampuni ya Longping Agriscience LTD na Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde mara baada ya mazungumzo yaliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Kwa upande Mkurugenzi Liang Shi amesema wamelenga kuanzisha mashamba ya darasa, kuwasaidia wakulima wazawa kwa mafunzo ya vitendo, kuanzisha vituo vya mauzo vitakavyoweka uwazi wa bei za mazao katika maeneo mbalimbali nchini.

Rais Samia ashiriki mkutano maalum wakuu wa nchi EAC
Binti azika kichanga kikiwa hai, adai hakujua kama anaujauzito