Bunge nchini Uganda limesema Bunge hilo litafungwa kuanzia wiki ijayo tarehe 28 Juni hadi tarehe 11 Julai ili kusafisha majengo ya Bunge, lengo likiwa ni kuzuia jengo hilo kuwa kitovu cha maambukizi ya Corona kutokana na idadi kubwa ya watu wanaolitembelea.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa mawasiliano na masuala ya umma katika Bunge hilo, Chris Obore imesema uamuzi huo umechukuliwa lengo la kupambana na maambukizi ya Covid 19.
Bunge la sasa la Uganda lina jumla ya wabunge 529 , mabali na wahudumu wa bunge, maafisa wa usalama, waandishi wa habari, na watoaji wa huduma mbalimbali.
Bunge la Uganda lilikuwa na majukumu makuu ya kusomwa kwa Bajeti, Hotuba y hali mbaya ya Taifa ambayo huwa inasomwa na Rais.
Hata hivyo mamia ambao walihudhuria matukio hayo wametakiwa kufanya vipimo vya corona na endapo watapatikana na maambukizi wametakiwa kujitenga wenyewe.
Mpaka sasa takriban watu 180 walipatikana na maambukizi ya corona kabla ya matukio haya mawili tofauti, 14 kati yao walikuwa ni Wabunge na 10 walikuwa ni wafanyakazi wa Bunge.