Mabingwa watetezi wa soka la vijana Mtibwa Sugar U-20 wamerejea mjini Morogoro na kupewa mapokezi ya kifahari baada ya vijana hao kuibuka kuwa mabingwa wa taji hilo dhidi ya Young Africans.

Kikosi cha Mtibwa Sugar U-20, kiliibuka na ushidni wa mabao 2-1 mwishoni mwa juma lililopita, Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam, na kutwaa taji hilo kwa mara ya tatu mfululizo.

Baada ya kuwasili mjini Morogoro, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Mtibwa Sugar Thobias Kifaru alizungumza na waandishi wa habari na kusema moja kati ya ahadi kubwa ambayo timu hiyo imeipata ni kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Martine Reuben Shigela, baada ya  kutoa ahadi ya kuwapatia viwanja kwa kila mchezaji aliyeshiriki michuano hiyo.

“Tunaishukuru Serikali ya mkoa kwa kutambua na kudhamini umuhimu wa soka la vijana kwa kuonyesha umuhimu mkubwa kwa hawa vijana kwani suala la kuwajali ni suala letu sote na sio kwa viongozi wa Mtibwa tu kwa kuwa wachezaji hawa wanatengeneza kizazi bora kijacho kwa manufaa ya timu yetu ya Taifa “Taifa Stars” amesema.

Aidha Thobias amesema kuwa wao kama viongozi wa Mtibwa wataendelea kuwajali na kuwatunza wachezaji hao huku wakitoa fursa kwa vijana hao kuonekana katika Ligi kuu Tanzania Bara na mashindano mbalimbali ndani na nje ya nchi.

“Mtibwa ni chuo cha soka hilo halina ubishi, Malengo yetu makubwa kama Uongozi wa Mtibwa ni kuona vijana wanajitangaza na kufika mbali zaid ya hapa walipo kwa sasa na hili tutalifanya kwa kuwapa nafasi katika kikosi chetu cha wakubwa ili wazidi kujitangaza na kutambulika zaidi nje ya Mipaka ya nchi” amesema.

Mtibwa Sugar iliandika rekodi ya kipekee kwenye sokala vijana U-20 kwa kufanikiwa kuwa timu ya kwanza kwenye michuano hiyo kuchukua taji hilo mara tatu mfululizo mwaka 2018, 2019 na 2021.

Uganda: Bunge lafungwa kwa wiki mbili
Serikali yajipanga kukomesha ukatili wa kijinsia katika vyombo vya habari