Shetani la mauaji limemvaa mhasibu mmoja mwenye umri wa miaka 35, ambaye alichukua uamuzi wa kuwachinja watu 14 wa familia yake wazazi wake, mkewe, watoto wake wa kike wawili, dada zake pamoja na watoto wao, mapema jana (Februari 28).

Kwa mujibu wa Polisi wa jiji la Mumbai nchini India ambapo tukio hilo lilifanyika, Husnain Werekar ambaye alikuwa anafanya kazi ya uhasimu katika kampuni inayofahamika kama ‘CA Firm’, alitekeleza tukio hilo la kinyama nyumbani kwake akitumia kisu kikubwa kukata makoromeo ya ndugu zake hao wa damu moja.

Husnain

Polisi wamewaeleza waandishi wa habari kuwa baada ya kufika katika nyumba hiyo, walikuta miili 14 ikiwa imelazwa sakafuni ikiwa imekatwa makoromeo. Pia, waliona mwili wa Husnain ukiwa umening’inia baada ya kujinyonga lakini kisu alichotumia kilikuwa bado mkononi mwake.

Polisi hao wameeleza kuwa, mwanae mwenye umri wa miezi mitatu tu aliyetajwa kwa jina la Umera, alikuwa kati ya watoto saba aliowaua kikatili.

Imeelezwa kuwa siku moja kabla, Husnain aliyekuwa anaishi na wazazi wake, watoto wake pamoja na dada zake ambao walikuwa hawajaolewa, aliwaalika pia dada zake watatu na watoto wake kwa ajili ya hafla ya pamoja ya kifamilia (family get-together).

Kamishna wa Polisi, Ashuton Dhumbre alisema kuwa wanaamini Husnain aliwapa kilevi ndugu zake hao kabla hajaanza kuwaua kikatili.

 

Polisi yatolea majibu taarifa za kukamatwa Maalim Seif (Audio)
Ridhiwani Amwaga mamilioni Shule za Chalinze