Uongozi wa Azam FC umeonyesha kuwa una thamini kwa kiasi kikubwa uhuru wa wachezaji wake.

Hali hiyo inatokana na uamuzi wa kutaka kuona wachezaji wake wanapiga kura katika uchaguzi Mkuu wa Jumapili Oktoba 25 kwa kuamua kuwasafirisha usiku.

Azam FC inashuka dimbani Alhamisi kuivaa Ndanda FC kwenye Uwanja wa Nangwanda kuwavaa wenyeji Ndanda FC.

Baada ya hapo, itaanza safari ili wachezaji wake wawe jijini Dar es Salaam mapema kujiandaa na suala la upigaji kura Jumapili.

“Lengo letu ni kuhakikisha wachezaji wetu wanapata nafasi ya kupiga kura kwa uhakika kwa kuwa ni haki yao,” alisema Saad Kawemba, mmoja wa wakurugenzi wa Azam FC.

Vumbi La Ligi Kuu Kutimka Tena Kesho
SDL Yapigwa Kalenda