Bingwa wa dunia wa mbio fupi duniani Usain Bolt ataanza kufanya mazoezi sambamba na kikosi cha klabu ya soka ya Borussia Dortmund ya nchini Ujerumani.

Mtendaji mkuu wa klabu hiyo ya Signal Iduna Park Hans-Joachim Watzke, amethibitisha taarifa za mwanariadha huyo kutoka nchini Jamaica, kwa kusema atawasili klabuni wakati wa maandalizi ya msimu mpya wa ligi.

Kabla ya kuthibitishwa kwa taarifa za Bolt kufanya mazoezi na kikosi cha Borussia Dortmund, baadhi ya vyombo vya habari nchini Ujerumani viliripoti kama taarifa hii kama tetesi.

Hata hivyo Watzke amesema suala hilo lilikua katika mipango yao ya siku nyingi na lilizungumza katika vikao vyao vya ndani, na mpaka wamefikia hatua ya kulitangaza hadharani wamepitia njia kadhaa.

“Tulizungumza katika vikao vyetu, na tulifanya maamuzi ya kimya kimya kutokana na umuhimu wa mwanariadha huyu ambaye ameendelea kufanya vyema katika michuano ya Olimpiki tangu mwaka 20008,” Alisema Watzke.

“Mtendaji mkuu wa kampuni ya vifaa vya michezo ya Puma Bjorn Gulden ambaye ni mjumbe wa bodi ya viongozi klabuni hapa, alileta wazo la Bolt kuwa sehemu ya mazoezi ya kikosi chetu na tulilipokea kwa mikono miwili. “Tuliona kuna umuhimu wa kufanya hivyo kutokana na sababu za kutanua wigo wa uhusiano kati yetu na mwanariadha huyo.

“Hakutaka kuwa sehemu ya mazoezi katika juma hili ambalo kikosi chetu kitakua na maandalizi ya mchezo wa ligi pamoja na ligi ya mabingwa barani Ulaya, lakini sisi tulipenda iwe hivyo,”

“Kutokana na hali hiyo tumepanga kuwa na Bolt katika mazoezi ya kikosi chetu wakati wa maandaalizi ya msimu mpya wa ligi kwa msimu wa 2017/18.”

The Gunners Wajizatiti Kwa Mesut Ozil
Magaidi wa Boko Haram ‘wamtishia nyau’ Trump