Mabingwa wa soka barani Ulaya klabu ya Real Madrid wameendelea kuhusishwa na mpango wa kutaka kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Argentina Sergio Kun Aguero.

Gazeti la The Mirror limeripoti kuwa, jina la mshambuliaji huyo wa Man city lipo kwenye orodha ya uongozi wa Real Madrid, licha ya kukabiliwa na kifungo cha kusajili kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Magwiji hao wa soka wa mjini Madrid wamekua wakifanya hivyo kwa kuamini kifungo cha kutosajili ambacho kilitolewa na FIFA mwezi mmoja uliopita, hakitowazuia kuendelea na mipango ya kufanya upembuzi wa kina na kuwafuatiliwa wanaodhamiria kuwasajili kwa baadae.

Mchezaji mwingine ambaye anadaiwa kuwa kwenye orodha ya Real Madrid ni mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang, ambaye huenda akaruhusiwa kuondoka mwishoni mwa msimu ujao.

Aguero amesaliwa na mkataba wa miaka mitatu na nusu, na tayari ameanza kuonyehsa kuchoshwa na falsafa za meneja mpya wa Man city Pep Guardiola, ambazo tayari zimeshamuweka nje ya kikosi cha kwanza kwa zaidi ya mara tatu.

Video: Swali la Mbowe kwa Waziri MKuu Bungeni
Aaron Ramsey: Tutakua Wa Kwanza Kuwafunga Spurs