Diamond Platinumz anatajwa na mashabiki wengi wa muziki nchini kama kipimo cha juu zaidi cha mafanikio katika tasnia ya Muziki wa Bongo Fleva kwa sasa, japo yeye hudai kuwa na njaa ya kuvuka boda kila kukicha.

Jana katika kipindi cha Friday Night Live cha EATV, Shabiki mmoja alimuuliza msanii mkubwa na mkongwe kwenye muziki, Bushoke kuwa ni lini ataweza kufika kiwango alichopo Diamond kwenye muziki kwa sasa.

Mkali huyo wa ‘Mume Bwege’, hakutaka swali hilo limpite japo mtangazaji hakulitilia maanani wakati linapita kwenye ‘screen’.

“Kuna mtu hapa anauliza ni lini nitafikia level za Diamond… Mimi siwezi kuwa nDiamond. Mimi nitabaki kuwa Bushoke na Diamond atabaki kuwa Diamond,” alisema.

Bushoke ambaye amekuwa kimya kwa muda mrefu aliwaahidi mashabiki wake kuwa hivi karibuni ataingia studio kupika wimbo mkubwa kwa ajili yao.

Madee afunguka baada ya kumsikia Dogo Janja akimchana
Kinachojiri Uganda baada ya Mpinzani wa Museveni kutiwa Mbaroni tena