Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki imesema kuwa mataifa 95 yamejitolea kutoa msaada katika kazi ya kusafisha, kuondoa mabaki na kuvunja majengo yanayoonekana kuhatarisha usalama wa watu kurejesha eneo lililoathirika katika hali ya kawaida.
Taarifa hiyo imesema zaidi ya waokoaji 110,000 watakuwa tayari sambamba na upatikanaji wa vifaa muhimu kwa ajili ya kazi hiyo ikiwamo trekta na mashine za kuchimbia.
Hali ya baridi kali, ndiyo iliyoongeza ugumu wa utafutaji wa majeruhi na kufifisha matumaini ya kupatikana majeruhi zaidi pamoja kuwa timu ya wataalamu walisema, kuna uwezekano wa majeruhi kuhimili kwa muda wa wiki moja au zaidi.
Tayari makundi mbalimbali yamejitolea kutoa msaada kwa waathirika, ikiwa ni pamoja na kuwapatia nguo, chakula na damu kwa majeruhi, huku ikisemekana kuwa zaidi ya watu milioni 4.1 Kaskazini Magharibi mwa Syria.
Ilielezwa kuwa zaidi ya watu milioni 13.5 nchini Uturuki wameathiriwa na tetemeko hilo katika maeneo ya Magharibi, Mashariki na Kusini katika miji ya Adana, Diyarbakir Malatya na Hatay.
Hata hivyo matumaini ya kupata watu walio hai katika vifusi vilivyotokana na tetemeko lililotokea chini Uturuki na Syria yamefifia huku idadi ya vifo inayoripotiwa ikiendelea kuongezeka na kufikia 41,987.