Takwimu za benki ya Dunia zinasema kati ya watu milioni 88 hadi 115 wanasukumwa katika umasikini kutokana na Janga la UVIKO 19 ikiwa wengi wanatokea Kusini mwa Jangwa la Sahara na Nchi za Asia.

Makadirio yanaeleza kuwa mwaka 2021 idadi inatarajiwa kuwa kubwa kati ya 143 na 163 ambapo watu hawa watajiunga na kundi la watu Bilioni 1.3 ambao tayari wanaishi katika Umasikini wa hali ya juu.

Wakati umasikini ukisongea kwa watu Huko nchini Misri Serikali imetangaza kuwa watumishi wa Umma ambao hawajapata chanjo dhidi ya Corona hawataruhusiwa kuingia kwenye majengo ya Serikali kuanzia Novemba 2021.

Hadi sasa Misri imetoa Chanjo kwa raia zaidi ya milioni 30 na kuanzia tarehe 15 Novemba wasiopata chanjo watalazimika kufanyiwa vipimo kila wiki ili waruhusiwe kuingia Kazini.

Kupitia ujumbe wake maalum kwa siku kimataifa ya kutokomeza umasikini Duniani Katibu mkuu Wa Umoja wa mataifa tarahe 17 Oktoba 2021 amesema Corona ni janga juu ya janga kwa watu masikini duniani kutokana na sababu kuu mbili. 

“Mosi ndio walio katika hatari kubwa ya kupata virusi hivyo na ndio watu wasio na fursa ya huduma bora za afya. Pili makadirio ya hivi karibuni yanaonyesha kwamba janga la COVID-19 linaweza kuwasukumua hadi watu milioni 115 kutumbukia kwenye umasikini mwaka huu, ikiwa ni ongezeko la kwanza la umasikini kwa miongo kandhaa, huku wanawake wakiwa katika hatari kubwa zaidi kwa sababu ndio walio na uwezekano mkubwa wa kupoteza kazi zao na pia kukosa ulinzi wa hifadhi ya jamii.” 

Guterres amesisitiza kwamba hizi ni nyakati ngumu ambazo zinahitaji juhudi za hali ya juu kupambana na umasikini na janga la COVID-19 linahitaji juhudi imara za pamoja kulikabili. 

Amehimiza kwamba “Serikali lazima zisongeshe mabadiliko ya kiuchumi kwa kuwekeza kwenye ujikwamuaji endelevu na unaojali mazingira.Tunahitaji kizazi kipya chenye mipango ya ulinzi wa hifadhi ya jamii ambayo itawalinda pia watu wanaofanya kazi katika sekta zisizo rasmi.” 

Kwa mantiki hiyo amesema “Kushikamana kwa pamoja kwa ajili ya maslahi ya kila mtu ndio njia pekee ya kujikwamua vyema na salama kutoka kwenye janga hili.” 

Katika siku hii ya kimataifa ya kutokomeza umasikini ambayo huadhimishwa kila mwaka Oktoba 17, ametoa wito wa kusimama Pamoja na kushikamana na watu wanaoishi katika umasikini wakati wote wa janga la COVID-19 na baada ya janga hilo. 

KMC FC: Tupo tayari kuikabili Young Africans
Biashara United waishukuru TFF, TPLB