Pamoja na kutokea kwa ajali ya ndege mali ya Precision Air Novemba 6, 2022 Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imesema Uwanja wa Ndege wa Bukoba upo salama huku ikiwatoa hofu Watanzania wanaotumia usafiri wa Ndege kuelekea Kagera.

Amesema ajali hiyo iliyotokea Novemba 6 mwaka huu baada ya ndege hiyo kuanguka Ziwa Victoria karibu na uwanja huo na kusababisha vifo vya watu 19 na 24 kunusurika ilikuwa bahati mbaya huku akisema katika sekta ya anga tukio lolote linalotokea ni funzo ili kuhakikisha halijitokezi kwa mara nyingine.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania – TCAA, Hamza Johari akizungumza na waandishi wa habari.

Kauli hiyo, imetolewa hii leo Novemba 9, 2022 na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu majukumu ya kiufundi ya TCAA na ajali ya ndege ya shirika la Precision Air iliyosababisha vifo na majeruhi.

Amesema, “Kampuni ya Precision imeanza kwenda Bukoba tangu mwaka 1992 ikianza na ndege ya abiria saba na mwaka 1996 wakaongeza nyingine ya abiria nane pamoja na kuwepo ya ziada ya abiria 11 na Mwaka 1998 walikuja ma ndege ya kubeba abiria 18 huku mwaka 2008 walianza safari ya kubeba abiria wengi.”

TCAA inasema Kiwanja cha ndege cha Bukoba ni salama.

Johari ameongeza kuwa, “Kama kiwanja cha ndege cha Bukoba ni hatarishi tungekuwa na mlolongo wa takwimu hizi, mwaka 1980 Air Tanzania ilianza safari za kwenda Bukoba na abiria 19 na mwaka 2017 ikaendelea na safari sasa TCAA tusipoweka sawa wasafiri wataamini uwanja wa Bukoba sio salama, ajali iliyotokea ni bahati mbaya.”

Uwanja wa ndege wa Bukoba una urefu wa mita 1500 na upana wa mita 30, ukiwa na uwezo wa kuhudumia ndege zenye uzito wa tani 29 wakati Ndege iliyopata ajali ilikuwa uzito wa tani 18.3.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Novemba 10, 2022 
Msafara wa Jeshi washambuliwa, 14 wafariki