Uamuzi wa Rais Magufuli kuzuia safari za nje kwa watumishi wa umma mpaka kwa kibali maalumu kutoka kwake au kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa unaonekana kukwamisha utendaji wa Bunge na mahakama.

Agizo hilo huenda likakwamisha safari za baadhi ya wabunge waliotakiwa kuhudhuria mkutano wa Agoa nchini Marekani ambao ni matunda ya kuanzishwa kwa mpango wa ukuzaji wa fursa za kiuchumi Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kuingiza katika soko la Marekani bidhaa 7,000 tofauti bila kutozwa ushuru.

Tanzania Daima ilipata nafasi ya kuongea na mbunge mmoja ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema, walipaswa kuondoka leo kwenda kuhudhuria mkutano huo, lakini hadi jana walikuwa hawajaona dalili ya kusafiri kwa kuwa spika wa bunge, Job Ndugai, alikuwa hajapata kibali kutoka Ikulu.

Spika Ndugai alikiri kupata taarifa za kusafiri kwa wabunge hao jana nayeye kufanya utaratibu wa kuwaombea kibali na mpaka jana hakuwa amepata majibu hivyo hana uhakika kuhusu safari hiyo, naye alisema,

‘’Sijajua ilikuwaje jambo hili halikufanyiwa utaratibu mzuri na kufika kwangu mapema mimi nilishatimiza wajibu wangu ila sijui kama wataweza kusafiri au hawatawezi’’.

Naye Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), alisema suala la kubana matumizi ni jema lakini kuna mazingira mengine ambayo shughuli haigharamiwi  hata kwa shilingi za serikali, huvyo ni vyema kuruhusu moja kwa moja wahusika kusafiri bila kusubiri kibali.

JPM atengua uteuzi wa Prof. Mlawa LAPF, Avunja Bodi
Video: Waziri Mkuu apokea michango ya sh. milioni 40, Waathirika Kagera