Wamiliki wa klabu ya Liverpool wamefutilia mbali bei mpya ya tiketi inayogharimu pauni 77 na kuomba msamaha kuhusu usumbufu uliosababishwa na tangazo la kiingilio kipya.

Maelfu ya mashabiki waliondoka katika uwanja wa Anfield kunako dakika ya 77 katika mchezo dhidi ya Sunderland ili kupinga ada hiyo mpya.

Katika kurudisha bei ya awali wamiliki wa klabu hiyo Fenway Sport waliwaambia mashabiki wao kwamba ‘wamepata ujumbe’.

Tiketi hizo sasa zitauzwa kwa pauni 59 kwa kila moja.

Liverpool fans managed to get the club to perform a U-turn on their plans to introduce £77 tickets

Mmiliki wa klabu ya Liverpool, John W Henry, mwenyekiti Tom Werner na rais wa FSG, Mike Gordon walitoa barua ya wazi wakielezea mabadiliko hayo, kufuatia kile walichokitaja kuwa wiki ya kutatiza.

”Sisi watatu tumeshangazwa na madai kwamba hatuwajali mashabiki wetu, kwamba sisi ni walafi na kwamba tunajaribu kujilimbikizia faida za kibinafsi bila kujali klabu hiyo,”alisema John W Henry.

Jose Mourinho Awaweka Sokoni Juan Mata, Marouane Fellaini
Ronaldo Awajibu Wanaomzulia Safari Ya Kuondoka Madrid